Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:46

Ghasia za zuka Abyei kura ya maoni ikiendelea Sudan


Askari wa Sudan Kusini akisindikiza msafara wa watu wanaorudi kutoka kaskazini kuelekea Abyei.

Maafisa wa Sudan wanasema watu wapatao 36 wameuwawa katika siku 3 za mapigano makali katika wilaya iliyo na mzozo wa Abyei huku wapiga kura wakiendelea kufurika katika vituo vya kupigia kura katika tukio la kihistoria la kura ya maoni ya Sudan Kusini.

Viongozi wa makabila ya kaskazini ya Misseriya na wale wa kusini Ngok Dinka waliendelea kutupiana shutuma jumatatu juu ya kuendelea kwa ghasia katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei ambalo linapiganiwa kati ya mpaka wa kaskazini na kusini.

Msemaji wa umoja wa mataifa Martin Nesirky amesema askari walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameongeza doria katika eneo la Abyei. Amesema Umoja wa Mataifa umeguswa sana na ghasia na wapo katika hatua ya kuthibitisha idadi ya majeruhi.

XS
SM
MD
LG