Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 03:03

Wasudan wapiga kura ya kihistoria juu ya Uhuru wao

Wanawake wa Sudan kusini wakisimama kwenye mstari mrefu wakisubiri kupiga kura katika kura ya maoni katika mji mkuu wa Juba,Sudan ya kusini. Jan. 9, 2011.
Wanawake wa Sudan kusini wakisimama kwenye mstari mrefu wakisubiri kupiga kura katika kura ya maoni katika mji mkuu wa Juba,Sudan ya kusini. Jan. 9, 2011.

Zoezi la kura ya maoni ya kihistoria huko Sudan Kusini ilianza Jumapili, kukiwepo na ripoti za maelfu ya wapiga kura wakijitokewa kwa furaha na shangwe.

Maelfu na maelfu ya wakazi walisimama usiku mzima nje ya vituo vya kupiga kura ili kua miongoni mwa wapiga kura wa kwanza katika uchaguzi utakao amua ikiwa Sudan ya kusini na kaskazini zitabaki kua taifa moja au kugawika na kuwa mataifa mawili.

Upigaji kura utaendelea kwa wiki nzima na inatazamiwa kwamba wa Sudan wa kusini watapiga kura kwa wingi mkubwa kutaka uhuru wao.

Rais wa Sudan kusini Salva Kiir akipiga kura katika kura ya maoni mjini Juba, Sudan kusini, Sunday, Jan. 9, 2011.
Rais wa Sudan kusini Salva Kiir akipiga kura katika kura ya maoni mjini Juba, Sudan kusini, Sunday, Jan. 9, 2011.

Kundi la wapigaji kura na wanawake walishangilia na kuimba baada ya rais wa Sudan kusini Salva Kiir, kupiga kura yake katika mji mkuu wa Juba Jumapili asubuhi. Bw. Kiir alisema huu ni wakati wa kihistoria kwa wananchi wa Sudan kusini walikua wanausubiri kwa muda mrefu.

Upigaji kura unaonekana ulifanyika kwa utulivu, ingawa maafisa waliripoti mapambano kati ya watu wa makabila ya Misseriya na Ngok Dinka katika eneo linalogombaniwa lenye utajiri wa mafuta wa Abyei.

XS
SM
MD
LG