Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 04:19

Upigaji kura ya maoni waanza Sudan Kusini


Wananchi wa Sudan wakipiga kura.
Wananchi wa Sudan wakipiga kura.

Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir alielekea mji mkuu wa Juba na kuacha sanduku la kura kwa wananchi wa eneo hilo waliokuwa wakishangilia na kusubiri wakati wao kuingia kupiga kura

Wengi walikuwa wakilisubiri kwa usiku kucha na ilipofika asubuhi walizongwa na camera za waandishi wa habari toka duniani kote ambao walikusanyika katika eneo la makumbusho ya John Garang kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za tukio hilo.

Upigaji kura utakaoendelea kwa juma zima ni hitimisho la mkataba wa amani wa mwaka 2005 kati ya Sudan ya kusini na ile ya Kaskazini. Baada ya miaka kadhaa ya majadiliano yaliyosimamiwa na Marekani, pande za kusini na kaskazini zilisaini mkataba wa kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 21 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu milioni mbili wa upande wa kusini na zaidi ya milioni nne kuyakimbia makazi yao.

Kati ya asasi zinazofuatilia upigaji kura huo, ni taasisi ya Carter Center chenye makazi yake jijini Atlanta Marekani. Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan wameongoza ujumbe wa kituo hicho katika eneo la kusini mwa Sudan.

Bw. Carter na Bw. Annan, jana walitembelea vituo kadhaa vya upigaji kura huko Juba na kukutana na wafanyakazi wa vituo hivyo na pia kujionea hali ya furaha iliyotawala eneo zima la kusini.“Hii ndio demokrasia katika uhalisia wake, ambapo watu wanachagua ni nani awaongoze na ni vipi waongozwe” Alisema Bw. Annan.

Upigaji kura wa Sudan ya kusini utachukua muda wa juma moja, mpaka Januari 15 na itachukua takriban mwezi mzima kabla matokeo rasmi kutangazwa. Mpaka mwisho wa siku ya kwanza ya upigaji kura huo, kile kilichotiliwa mashaka kama kingeweza kutokea sasa chaonekana kama jambo la kawaida na la kufurahisha.

XS
SM
MD
LG