Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 12:43

Rais Bashir atatembelea Sudan ya Kusin


Eamon Omordha, (kulia), Naibu mkurugenzi wa idara ya mfumo wa uchaguzi ya Umoja wa Mataifa anamkabidhi Hakimu Chan Reec Madut, (kushoto), mwenyekiti wa tume ya kura ya maoni ya Sudan ya Kusini, wakati wa sherehe mjini Juba.
Eamon Omordha, (kulia), Naibu mkurugenzi wa idara ya mfumo wa uchaguzi ya Umoja wa Mataifa anamkabidhi Hakimu Chan Reec Madut, (kushoto), mwenyekiti wa tume ya kura ya maoni ya Sudan ya Kusini, wakati wa sherehe mjini Juba.

Mwanachama maarufu wa chama tawala nchini Sudan, Rabie Abdelati Obeid, anasema Rais Omar al-bashir atatembelea kusini mwa nchi kabla eneo hilo kupiga kura ya maoni Januari 9, juu ya uhuru wa eneo hilo.

Bw. Obeid, alisema ziara ya rais itaonesha dhamira ya serikali ya kuendelea na uhusiano mzuri na kusini, hata kama eneo hilo lenye utawala wa mamlaka ya ndani hivi sasa linapiga kura ya kuwa na uhuru kamili.

Bw. Obeid alisema bwana Bashir atahakikisha matayarisho ya upigaji kura yanafanywa na atakutana na viongozi wa kusini kuzungumzia njia za kuhakikisha kura ya maoni inafanyika kwa njia ya huru, wazi na haki. Tarehe kamili ya ziara ya Rais haijajulikana.

Katika hotuba yake siku ya Ijumaa, Bw. Bashir alisema serikali yake imejiandaa kikamilifu kwa upigaji kura na itakubali matokeo yake.

Kura ya maoni ni sehemu muhimu ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza zaidi ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Sudan kaskazini na kusini.

XS
SM
MD
LG