Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 05:34

Strauss-Kahn ajiuzulu IMF


Dominique Strauss-Kahn

Aendelea kukanusha madai ya ubakaji na anatazamiwa kufika mahakamani Alhamisi kuomba tena dhamana

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa IMF Dominique Strauss-Kahn amejiuzulu wadhifa wake katika shirika hilo, akisema anahitaji muda zaidi kupambana na mashitaka ya ubakaji yanayomkabili.

Katika barua iliyowasilishwa Jumatano usiku kwa Bodi ya Utendaji ya IMF Strauss-Kahn alisisitiza kuwa hana hatia katika mashitaka yanayomkabili.

Alisema anajiuzulu kulinda heshima ya shirika ambalo amelifanyika kazi kwa nguvu zake zote.

Kujiuzulu huko kumetokea huku mawakili wake wakitarajia kufika katika mahakama kuu ya jimbo la New York leo kuomba tena dhamana kwa ajili ya mteja wao.

XS
SM
MD
LG