Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:59

Strauss-Kahn afunguliwa mashitaka saba


Dominique Strauss-Kahn, akiwa na wakili wake Benjamin Brafman, katika mahakama ya Manhattan New York
Dominique Strauss-Kahn, akiwa na wakili wake Benjamin Brafman, katika mahakama ya Manhattan New York

Atalazimika kukabidhi hati zake za kusafiria wakati kesi yake inaendelea

Mkuu wa zamani wa shirika la fedha la kimataifa IMF Dominique Strauss-Kahn amefunguliwa mashitaka saba ya uhalifu wa kingono katika mahakama ya mjini New York kufuatia madai kuwa alimbaka mwanamke mmoja msafisha chumba katika hoteli moja ya mjini hapo.

Strauss-Kahn, ambaye alikuwa rumande katika gereza la Rikers Island tangu akamatwe, pia amepewa dhamana ya dolla millioni moja fedha taslimu, na kuweka dhamana mali yenye thamani ya dolla millioni tano. Atalazimika kubaki nyumbani kwake mjini New York.

Hata hivyo, hakuachiliwa huru leo. Wakili wake alisema katika mkutano mfupi na waandishi wa habari kuwa Strauss-Kahn amerudishwa Rikers Island baada ya kutoka na mahakamani na huenda akaachiliwa huru Ijumaa.

Mahakamani Strauss-Kahn alifunguliwa mashitaka mawili ya uhalifu wa kingono katika kiwango cha juu kabisa, kosa moja la jaribio la ubakaji na mashitaka mengine yanayohusiana na mambo yaliyotokea katika chumba chake kwenye hoteli ya Sofitel mjini New York, Jumamosi iliyopita.

XS
SM
MD
LG