Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:15

Mkuu wa IMF akamatwa New York


Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Dominique Strauss-Kahn atiwa nguvuni New York Jumamosi
Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Dominique Strauss-Kahn atiwa nguvuni New York Jumamosi

Adaiwa kujaribu kumbaka mwanamke msafisha vyumba katika hoteli moja ya mjini New York

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, Dominique Strauss-Kahn anashikiliwa kwa mahojiano na polisi wa mjini New York kwa madai ya kujaribu kumbaka mwanamke msafisha vyumba katika hoteli moja ya Manhattan, kulingana na kamishna wa polisi wa New York Paul Browne.

Polisi walimtoa Strauss-Kahn kutoka katika ndege ya Air France kwenye uwanja wa kimataifa wa JFK akiwa tayari kuelekea Ufaransa baada ya tukio hilo analodaiwa kulifanya. Alitiwa nguvuni na kupelekwa Manhattan, New York, kwa mahojiano.

Saa chache kabla ya hapo, polisi wanasema, Strauss-Kahn alijaribu kumlazimisha mwanamke msafisha vyumba kufanya naye mapenzi katika chumba chake, lakini mwanamke huyo aliweza kumtoka na kukimbia. Wafanyakazi wa hoteli walipiga simu polisi, lakini hadi walipofika hapo mkuu huyo wa IMF alikuwa tayari amekwishaondoka, lakini aliwacha simu yake ya mkononi hotelini hapo.

Polisi waligundua kuwa mkuu huyo wa IMF alikuwa katika ndege uwanja wa JFK ikiwa tayari kutoka nje ya nchi.

Strauss-Kahn ambaye aliwahi kuwa waziri wa fedha wa Ufaransa, mbunge na professa wa uchumi aliteuliwa kuiongoza IMF mwaka 2007. Ingawa hajatangaza rasmi lakini anatazamiwa kuingia katika kinyang'anyiro cha urais kupambana na Rais Nicolas Sarkozy katika uchaguzi wa Ufaransa mwakani.

Hajafunguliwa mashitaka yoyote rasmi mpaka sasa.

XS
SM
MD
LG