Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:48

Mkuu wa IMF atakana mashitaka


Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Dominique Strauss-Kahn
Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Dominique Strauss-Kahn

Anatazamiwa kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashitaka rasmi

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Dominique Strauss-Kahn, anatazamiwa kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashitaka rasmi mjini New York baada ya polisi kumtia nguvuni kwa madai ya kujaribu kumbaka mwanamke mmoja katika hoteli mjini New York.

Wakili wa Bwana Strauss-Kahn anasema mkuu huyo wa IMF atakana mashitaka.

Alikamatwa Jumamosi usiku akiwa ndani ya ndege ya shirika la Air France kwa safari ya kwenda Ufaransa. Polisi wanasema saa chache kabla ya hapo Strauss-Kahn alijaribu kumbaka mwanamke mmoja msafisha chumba katika hoteli ya Sofitel mjini New York.

Mwanamke huyo ambaye angali anahojiwa na polisi anadai kuwa aliingia chumbani kwa Strauss-Kahn kufanya usafi akidhani hakuna mtu ndani. Lakini ghafla, anasema, Strauss-Kahn alitokea chumba kingine akiwa uchi na kujaribu kumvuta afanye naye mapenzi. Mwanamke huyo aliweza kuponyoka na kukimbia kuripoti kwa maafisa wa hoteli.

Haifahamiki kama Bwana Strauss-Kahn kama afisa wa juu wa shirika la kimataifa ana kinga ya kidiplomasia lakini polisi wanasema hajasema lolote kuhusu kudai kinga hiyo

XS
SM
MD
LG