Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 02:50

Somalia : Farmajo asema hataki tena nyongeza ya miaka miwili


Rais Mohamed Abdullahi Farmajo
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu Farmajo anasema hataki tena nyongeza ya miaka miwili kwa muhula wake wa urais

Rais amesema amekubaliana na shinikizo la ndani na la kimataifa kuachana na azimio lenye utata juu ya muda ya kuongezewa lililopitishwa na Baraza Kuu la Bunge la nchi hiyo.

Katika hotuba kwa njia ya televisheni, Mohamed alisema atafika mbele ya bunge siku ya Jumamosi, kuwaomba wabunge kurejesha makubaliano ya mwaka 2020 kati ya serikali kuu na viongozi wa majimbo matano pamoja na Gavana wa Mogadishu.

Mkataba unaojulikana kama “makubaliano ya Septemba 17” yalitoa wito wa uchaguzi wa wabunge kupitia uchaguzi usio wa moja kwa moja.

Wabunge baada ya hapo wangemchagua rais. Baraza kuu la bunge lilibatilisha makubaliano hayo April 12, na kuipa mihimili miwili ya utendaji na bunge miaka miwili mingine ili kuandaa uchaguzi mkuu.

Mohamed alitia Saini azimio hilo kuwa sheria hapo April 13. Muda wa rais kuwepo madarakani ulimalizika Februari 8 mwaka 2021, wakati mamlaka ya bunge yalimalizika Disemba 27 mwaka 2020.

Ikiwa bunge litaidhinisha ombi la Rais siku ya Jumamosi, litabadilisha ongezeko la miaka miwili lililowekwa.

XS
SM
MD
LG