Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 09:56

Rais wa zamani amshutumu Farmajo kutekeleza shambulizi dhidi yake


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed (AP Photo/Kevin Hagen).
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed (AP Photo/Kevin Hagen).

Kiongozi wa zamani wa Somalia amemshutumu mrithi wake, Rais Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu Farmajo kwa kupanga shambulizi lililofanywa na wanajeshi nyumbani kwake hapo Jumapili, huku mgawanyiko ukiongezeka juu ya kuongezewa muda kwa Rais aliyepo madarakani.

Shutuma za Rais wa zamani wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud dhidi ya Mohamed kwenye mtandao wa Twitter, ambazo hazikujumuisha maelezo ya kina au uthibitisho, zimekuja wakati vikundi ndani ya vikosi vya usalama vya Somalia vikirushiana risasi katika mji mkuu Mogadishu.

Mzozo huo unaibuka kufuatia Mohamed kusaini sheria katikati ya mwezi Aprili, akiongeza mamlaka yake kwa miaka miwili, suala ambalo litaweza kuvuruga vikosi vya usalama kutoka kwenye mapigano yao yanayoungwa mkono kimataifa dhidi ya waasi wa al-Shabaab wenye uhusiano na al-Qaida katika taifa hilo lililopo pembe ya Afrika.

Msemaji wa serikali hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni juu ya shutuma za Mohamud, ambaye aliondoka madarakani mwaka 2017.

Lakini waziri wa usalama wa ndani, Hassan Hundubey alikanusha kwamba serikali ilikuwa imevamia nyumba ya rais huyo wa zamani, kulingana na shirika la Habari la taifa nchini Somalia.

XS
SM
MD
LG