Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 14:24

Mapigano yazuka Mogadishu dhidi ya jeshi na wanajeshi wanaounga mkono upinzani


Rais wa Somalia President Mohamed Abdullahi Farmajo

Milio ya risasi ilisikika hapa na pale katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, Jumapili, baada ya vikosi vyenye uhasama kupambana kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo kuhusu uchaguzi.

Mashuhuda na wakazi wamesema mapigano yalitokea baina ya vikosi vya serekali ya rais Monamed Abdullahi Mohamed, anayefahamika kama Farmajo, na wanajeshi wa jeshi la Somalia, wanao egemea kwa viongozi wa upinzani.

Wakati wakazi walipokuwa wanafungua funga zao za mwezi mtukufu wa Ramadhan, muda wa jioni mapigano yalianza katika makutano ya barabara maarufu ya jiji la Mogadishu.

Shuhuda ambaye hakutaka kutajwa kwa sababu za kiusalama, amesema aliona wanajeshi wa serekali, na vikosi vinavyo hasimiana, wakifyatuliana risasi pamoja na maguruneti yaliyotumia roketi.

Hakukuwa na taarifa kuhusiana na vifo vilivyo tokea.

Viongozi wa serekali na upinzani wamekuwa wakipingana kutokana na uamuzi wa Aprili 12 uliofanywa na Bunge la chini la kuongeza muda wa serekali ya sasa kwa kipindi kingine cha miaka miwili baada ya mazungumzo ya uchaguzi kuvunjika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG