Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:22

Daktari Bingwa wa ngozi Somalia auawa


Daktari bingwa wa ngozi nchini Somalia ambaye alitoa huduma ya matibabu bure kwa maskini alipigwa risasi na kuuawa Alhamisi asubuhi nje ya nyumba yake mjini Mogadishu, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Somalia.

Daktari Hasan Osman Issa, anayefahamika zaidi kama Dkt. Burane, aliuawa na watu wenye silaha nyumbani kwake katika mji wa Al-Baraka katika mji mkuu wa Somalia kwenye wilaya ya Hodan, kulingana na ripoti.

VOA haikuweza kuwapata polisi kwa maelezo zaidi.

Burane alianzisha na kuendesha kliniki inayoitwa jina lake la utani.

Rais wa chama cha Madaktari wa Somalia, Mohamed Yusuf Hassan, alimsifu Burane kwa ukarimu wake.

"Daktari mzuri ameondoka nchini," alisema Hassan, ambaye pia anaongoza Hospitali ya Dar es Salaam. "Kama madaktari, wasiwasi wetu leo ni kwa mtu ambaye alifanya kazi kwa bidii kwa watu maskini" na kushughulikia magonjwa ya ngozi.

Hassan alisema kifo cha daktari huyo wa ngozi kinaleta "wasiwasi wa pekee”. Ikiwa Burane aliuawa, ni nani atakayepona? Hili sio jambo tunaloweza kukubali. Lazima tuandamane. Lazima tufanye kila njia kutatua maswala kama haya.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na mauaji hayo hadi mwishoni mwa siku ya Alhamisi nchini Somalia. Wiki iliyopita, Mohamed Abdi Ahmed, kamishna wa wilaya ya jiji la Hamar Jajab, aliuawa vivyo hivyo.

XS
SM
MD
LG