Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:02

Siku ya Mashujaa Marekani yawaenzi waliofariki wakitumikia jeshi lake


Sgt. Tim Chambers wa Jeshi la Majini la Marekani akitoa heshima mbele ya walioshiriki katika mkusanyiko wa maandamano ya waendesha pikipiki wa "Rolling to Remember" May 29, 2022, mjini Washington.
Sgt. Tim Chambers wa Jeshi la Majini la Marekani akitoa heshima mbele ya walioshiriki katika mkusanyiko wa maandamano ya waendesha pikipiki wa "Rolling to Remember" May 29, 2022, mjini Washington.

Siku ya Mashujaa mwaka huu, sikukuu ya serikali kuu, imeangukia Jumatatu, Mei 30.

Masoko ya fedha yamefungwa, na Rais Joe Biden atahudhuria maadhimisho hayo katika Makaburi ya Kitaifa ya Arlington.

Gwaride la Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa mjini Washington linarejea Jumatatu huko Mtaa wa Constitution Avenue, baada ya kutofanyika kwa miaka miwili kwa sababu ya janga la COVID.

Wamarekani wengi wanaadhimisha siku hii kwa kutembelea maeneo ya kumbukumbu ya mashujaa au kutembelea makaburi na kuweka maua.

Mjini Washington, wapanda pikipiki wamekuwa ni washiriki wa kawaida kuonekana siku ya Kuwakumbuka Mashujaa. Mwaka huu tukio la wapanda pikipiki limeitwa “Rolling to Remember” na limepanua ujumbe wake kuongeza ufahamu juu ya janga la mashujaa wengi kujiua.

Rolling to Remember imesema katika tovuti yake kuwa “maandamano ya wapanda pikipiki” Jumamosi ndani na kuzunguka mji wa Washington yalifanyika ili “kuongeza ufahamu wa masuala muhimu yanayo wakabili mashujaa wa taifa letu na wanataka hatua zichukuliwe kwa wanajeshi 82,000 wasiojulikana walipo, pamoja na kuongeza ufahamu wa mashujaa 22 ambao wanafariki kwa kujiua kila siku.

Kuna mikusanyiko ya familia nyingi na pikiniki Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa kama inavyojulikana kote kuwa ni kipindi cha kuanza rasmi msimu wa joto nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG