Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:41

Siku ya Uhuru wa Marekani : Hisia mseto juu ya maonyesho ya kijeshi


Rais Donald Trump akihutubia siku ya Sherehe za Uhuru wa Marekani mbele ya kumbukumbu ya jengo la Lincoln Memorial, Washington, Alhamisi, Julai 4, 2019.
Rais Donald Trump akihutubia siku ya Sherehe za Uhuru wa Marekani mbele ya kumbukumbu ya jengo la Lincoln Memorial, Washington, Alhamisi, Julai 4, 2019.

Maadimisho ya Uhuru wa Marekani mjini Washington DC, Alhamisi yalikuwa tofauti sana mara hii, kwa kuwepo maonyesho ya nguvu za kijeshi, na rais Donald Trump akitoa hotuba kuhusu uzalendo.

Hatua hiyo ya rais imesababisha hisia mseto kati ya wafuasi wa Trump na wakosoaji wake wanaomshutumu kwa kuingiza siasa katika siku kuu ya kitaifa, pamoja na kuharibu pesa za walipa ushuru.

Maadhimisho ya uhuru wa Marekani mwaka huu, yameshuhudia maonyesho ya ndege za kijeshi, pamoja na magari ya vita kwenye barabara za mjini Washington, kuonyesha nguvu za kijeshi za Marekani.

Rais Donald Trump, vile vile alitoa salamu za siku ya Uhuru wa Marekani kwa wananchi wote.

"tunasherehekea historia yetu na mashujaa waliotetea bendera yetu kwa kujivunia, wanawake na wanaume wa jeshi letu la Marekani, ” alisema Rais Trump.

Maadimisho hayo ya Julai 4 katika jiji kuu la Washington, kwa kawaida, huwa hayahusishwi na siasa. Lakini mwaka huu, yamekosolewa na duru za kisiasa kutokana na hatua ya Trump kuyafanya kuonekana ya kisiasa, wanaomkosoa wakitumia njia tofauti ikiwemo roboti inayofanana na Trump, inayotuma ujumbe wa Twitter kutoka chooni.

"Rais ameingiza siasa katiaka tukio lisilo la kisiasa kwa kujieka katikati na kuleta ndege na ala zingine za kivita. Amevifanya kuonekana kama vinywago vyake vya kuchezea ili ajisikie vizuri kwa gharama ya walipa ushuru," amesema Amanda Whitehead.

Hata hivyo baadhi ya wakosoaji wake wanahisi kwamba Trump ni rais anayependa mgawanyiko, asiyejua wala kujali tofauti kati ya kilicho kizuri na kibaya.

Lakini wafuasi wa Rais Trump wana maoni tofauti. Gil Daniels anasema : "Nadhani anafanya kila awezalo kusherekea nchi hii na kuwaunga mkono watu wake, hasa Wamarekani ambao wamesahauliwa."

Baadhi ya wafuasi wake wamefurahia hatua hiyo wakisema kwamba maadui wa Marekani, wanaofanya maonyesho ya silaha zao kila mara na kuongeza mabaya kuihusu Marekani na kujionyesha kama wanaweza kuiangamiza Marekani, kwa sasa wana uoga mwingi baada ya hatua ya Rais Trump kuonyesha uwezo wa kijeshi wa Marekani kwa dunia.

Baadhi ya watu wanaamini tangu Trump alipohudhuria sherehe za ukombozi wa Ufaransa mwaka 2017, amekuwa akitaka gwaride la kijeshi la Marekani kufanyika.

Mipango ya mwaka 2018 kuandaa gwaride hilo haikufaulu kufuatia hoja ya gharama ya kuandaa hafla hiyo, pamoja na ukosoaji mkubwa kuhusu hatua za kijeshi, maswala ambayo yametajwa na wakosoaji wake mwaka huu.

White house inasisitiza kwamba shabaha kubwa ya maadhimisho hayo ni kuhimiza uzalendo na wala sio siasa. Utawala wa Trump hata hivyo haujatoa hesabu ya gharama ya maadimisho hayo, ambayo inakadiriwa kuwa mamilioni ya dola.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG