Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 27, 2020 Local time: 21:25

Trump asema jaribio la kombora la Korea Kaskazini halimsumbui


Rais Donald Trump, kulia, na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe walipokutana na familia za wananchi wa Japan waliotekwa na majeshi ya North Korea, wakati rais alipofika katika kasri ya Akasaka Jumatatu, Mei 27, 2019, Tokyo.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema yeye binafsi halimsumbui suala la Korea Kaskazini kufanya majaribio ya kombora la balistika, akieleza “hilo siyo tatizo” iwapo majaribio hayo yamekiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Trump alitoa maoni hayo mjini Tokyo akiwa na Waziri Mkuu wa Japan, ambaye anamtizamo tofauti juu ya kurushwa makombora hayo, kama alivyoripoti mwandishi wa VOA.

Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa hakuna shaka kwamba Korea Kaskazini imejaribu makombora matatu ya balistika ya masafa mafupi mapema mwezi huu.

Satellite ya kibiashara imeonyesha picha ya alama ilioachwa na moshi angani uliotokana na makombora hayo.

Lakini hata hivyo ukisikiliza maoni ya Rais Donald Trump wakati wa ziara yake ya kiserikali Japan, hutotambua kabisa kwamba makombora hayo yalirushwa.

Donald Trump alisema kuwa : Ni siku nyingi sasa. Hapakuwa na jaribio la roketi. Hapakuwa na jaribio la silaha ya nyuklia. Kumekuwa na harakati chache kutoka katika eneo hilo.”

Trump aliendelea kupinga wafanyakazi wake, ambao wanasisitiza kuwa jaribio la makombora linakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG