Rais wa Marekani Joe Biden anatazamiwa kuzungumza siku ya Alhamisi kuhusu umuhimu wa kihistoria wa shambulio la mwaka jana dhidi ya bunge la Marekani lililofaywa na wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump.
Hotuba hiyo, katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa shambulio hilo, itaangazia Biden akizungumza kutoka kwenye jengo la bunge pamoja na Makamu wa Rais Kamala Harris.
Rais atazungumza juu ya ukweli wa kile kilichotokea, sio uwongo ambao wengine wameeneza tangu wakati huo na hatari ambayo imeleta kwa utawala wa sheria na mfumo wetu wa utawala wa kidemokrasia, msemaji wa White House Jen Psaki aliwaambia waandishi wa Habari katika mkutano wa Jumanne.
Pia ataadhimisha siku hiyo, kuwakumbuka mashujaa wa Januari 6, hasa wanaume na wanawake shupavu wa idara ya Polisi ambao walipigania kutetea Katiba na kulilinda bunge maisha ya watu waliokuwa huko.
Kwa sababu ya juhudi zao, demokrasia yetu ilistahmili mashambulizi kutoka kwenye kundi la watu wenye vurugu, na nia ya zaidi ya watu milioni 150 waliopiga kura katika uchaguzi wa urais hatimaye ilisajiliwa rasmi na Bunge.