Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 13:07

Viongozi wa Marekani waomboleza kifo cha McCain


Seneta McCain

Seneta wa Marekani John McCain ataendelea kukumbukwa kwa ushujaa, uzalendo wake na kwa kulitumikia taifa lake.

McCain ameaga dunia Jumamosi akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kupambana na ugonjwa wa saratani ya ubongo.

Historia fupi

Akiwa mtoto wa Admirali wa Marekani, McCain alifanya kazi ya urubani na kurusha ndege zilizofanya mashambulizi wakati wa vita ya Vietnam. Ndege yake ilitunguliwa na akakamatwa na wanajeshi wa Vietnam ya Kaskazini mwaka 1967, na kuvumilia mateso yaliyodumu kwa kipindi cha miaka mitano na kuishi maisha magumu jela kama mfungwa wa kivita.

Donald Trump

Rais Donald Trump ametuma ujumbe wa Tweet usemao : “Nina masikitiko makubwa na heshima zangu ziwaendee wanafamilia wa Seneta John McCain. Mioyo yetu na sala zetu ziwe pamoja nawe!”

Timu ya kampeni yake baadae ilituma salamu za rambirambi na kuwahimiza Wamarekani wote kutumia fursa hii kumkumbuka McCain na familia yake katika maombi yao kwa tukio hili lenye huzuni.

Mike Pence

Makamu wa Rais Mike Pence alituma ujumbe wa tweet, “Karen na mimi tunamuombea Seneta John McCain, Cindy na familia yao wikiendi hii. Mungu awabariki wote katika wakati huu mgumu.

Barack Obama

Rais mstaafu Barack Obama na mkewe Michelle Obama alitoa tamko akituma salamu za “rambirambi za dhati” kwa mkewe McCain, Cindy na familia yake.

Obama, ambaye alikuwa katika kinyang’anyiro cha urais akishindana na seneta wa Repulibikan na kumshinda, amesema pamoja na kuwa wao ni wa vizazi, historia na vyama tofauti, “tulikuwa tunaiangalia nchi hii kama mahali ambapo kitu chochote kinaweza kufanyika.

Bill Clinton na Hillary Clinton

Rais mstaafu Bill Clinton na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Hillary Clinton, ambaye alifanya kazi na McCain katika Baraza la Seneti la Marekani, amesema katika tamko lake kuwa yeye McCain “mara nyingi aliweka uchama pembeni kufanya kile alichofikiria ni bora kwa nchi hii na alikuwa haogopi kutekeleza ikiwa ni jambo sahihi lifanyike.

George W. Bush

Rais Mstaafu George W. Bush amemtaja McCain kuwa ni rafiki, ambaye “kwa yakini atamkosa.”

“Baadhi ya uhai unaong’aa, ni vigumu kuwaza watu hawa wakiaga dunia,” Bush amesema katika tamko lake.“Baadhi ya sauti ni zenye nguvu, ni vigumu kufikiria sauti hizo zikinyamaza.

Tanzia

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa McCain alikuwa amewaomba Obama na Bush kutoa tanzia yake katika maziko yake.

Baba ya Bush, Rais mstaafu George H.W. Bush, amemtaja McCain “ kuwa ni mzalendo wa kiwango cha juu, mtumishi wa umma mwenye ushujaa wa kipekee.”

“Wachache walijitolea zaidi au kuchangia zaidi, kwa maslahi ya raia wenzaka- na bila shaka watu wenye kupenda uhuru duniani,” Bush amesema katika tamko lake.

Mitch McConnell

Kiongozi wa wengi wa Baraza la Seneti Mitch McConnell amesema mfungwa wa kivita wa Vietnam “ alituonyesha jinsi uzalendo usio na mipaka na kujitolea kuwa ni fikra ambazo hazijapitwa na wakati, lakini vitu hivyo viwili vinajenga maisha yasiyo ya kawaida.

Paul Ryan

Spika wa Bunge Paul Ryan amesema kuwa kifo cha McCain ni kielelezo cha “siku ya masikitiko kwa taifa la Marekani,” ambalo limempoteza “shujaa wa vita na kiongozi.”

“John aliweka maadili mbele ya siasa. Aliweka taifa lake mbele kuliko maslahi yake binafsi,” Ryan amesema. “Alikuwa mwenye ushujaa zaidi katika mashujaa katika karne hii.”

Nancy Pelosi

Kiongozi wa chama cha Demokrat Nancy Pelosi amesema kuwa “taifa linamlilia” na kuelezakuwa McCain ni mzalendo, shujaa wa kipekee na asiyeogopa.”

John Kerry

Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani John Kerry, aliyefanya kazi na seneta katika Bunge na pia ni askari mwenzake katika Vita ya Vietnam, amesema kutofautiana kwao katika maoni juu ya vita na kukumbusha safari yao walipokuwa wanarejea Hanoi akiwa na McCain, ambapo wote walikuwa “wameweka misimamo ya pamoja.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG