Likiwa katika eneo la mnyanyuko katika makaburi ya taifa ya Arlington, makaburi ya kumbukumbu yaliyo karibu na mji wa Washington.
Kaburi hilo “ni eneo tukufu,” amesema Tim Frank, mwanahistoria katika eneo kubwa la makaburi ya jeshi nchini Marekani, walikozikwa zaidi ya wanaume an wanawake 400,000.
Ni eneo ambapo watu siyo tu wanaweza kumuenzi mwanajeshi asiyejulikana, aliyefariki katika Vita vya Kwanza vya Dunia, lakini wanajeshi wote, wanaojulikana na wasiojulikana majina yao, waliojitoa mhanga katika vita vilivyopiganwa na Marekani, Frank ameiambia VOA.
“Ni Ukumbusho wa Kijeshi mtukufu zaidi wa taifa “ na unalindwa wakati wote, ameongeza mwanahistoria Philip Bigler, mtunzi wa kitabu Tomb of the Unknown Soldier : A Century of Honor.
Siku ya Mashujaa, maarufu kama siku ya Armistice, ni sikukuu ya serikali kuu inayosheherekewa Novemba 11 kwa ajili ya kuwaenzi wanajeshi wa zamani.
Mwaka huu inafanyika pia kumbukumbu ya miaka 100 ya Makaburi ya Mwanajeshi asiyejulikana, asherehe ambazo zinavutia milioni kadhaa ya wageni kila mwaka.