Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 18:17

Hatua kubwa bado zahitajika katika mkutano wa hali ya hewa Glasgow


Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, na mwakilishi maalum wa Marekani kwa masuala ya hali ya hewa John Kerry, wakiwa pamoja na ujumbe wa Umoja wa Matiafa katika mkutano wa hali ya hewa Glasgow Scotland COP26, Jumanne 9 Nov. 2021.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, na mwakilishi maalum wa Marekani kwa masuala ya hali ya hewa John Kerry, wakiwa pamoja na ujumbe wa Umoja wa Matiafa katika mkutano wa hali ya hewa Glasgow Scotland COP26, Jumanne 9 Nov. 2021.

Mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa huko Glasgow umefanya hatua kadhaa ndogo muhimu katika kupunguza hewa chafu lakini bado ziko mbali na hatua kubwa zinazohitajika kupunguza ongezeko la joto duniani kwa malengo yanayokubalika kimataifa, uchambuzi mpya ulieleza.

Mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa huko Glasgow umefanya "hatua kadhaa za ndogo muhimu katika kupunguza hewa chafu lakini bado ziko mbali na hatua kubwa zinazohitajika kupunguza ongezeko la joto duniani kwa malengo yanayokubalika kimataifa, uchambuzi mpya na maafisa wakuu ulieleza Jumanne.

Na muda unazidi kuyoyoma kwa wiki mbili za mazungumzo waliongeza.

Rais wa mazungumzo ya hali ya hewa, Alok Sharma, aliwaambia mawaziri wa ngazi ya juu wa serikali katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuifikia miji mikuu na wakuu wao hivi karibuni ili kuona kama wanaweza kutoa ahadi kubwa zaidi kwa sababu "tumebakiza siku chache tu” aliongeza.

Mkutano wa kilele wa mwezi huu umeona maendeleo machache kiasi kwamba uchambuzi wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa wa ahadi mpya uligundua kuwa hazitoshi kuboresha hali ya ongezeko la joto siku zijazo. Walichofanya ni kupunguza pengo la utoaji wa hewa chafu ni kiasi gani cha uchafuzi wa hewa unaweza kusambazwa bila kufikia viwango vya hatari vya ongezeko la joto la sehemu ya kumi ya ya asilimia kulingana na uhakiki uliotolewa Jumanne.

Uchambuzi huo uligundua kuwa kufikia 2030, dunia itakuwa ikitoa tani bilioni 51.5 za kaboni dioksidi kila mwaka, tani bilioni 1.5 pungufu kuliko kabla ya ahadi za hivi karibuni. Ili kufikia kikomo kilichowekwa kwanza katika makubaliano ya hali ya hewa ya Paris ya mwaka 2015, ambayo yalitoka katika mkutano kama huo, ulimwengu unaweza tu kutoa tani bilioni 12.5 za gesi chafu ifikapo 2030.

​
XS
SM
MD
LG