Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:44

UN yachapisha rasimu ya uamuzi wa kisiasa wa mkutano wa Glasgow

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, na Mwakilishi Maalum wa Rais wa Marekani katika Masuala ya Mazingira John Kerry, wakiwa na wajumbe wa Marekani katika Kituo cha Marekani katika Mkutano wa Hali ya Hewa COP26 wa UN, Nov 9. 2021.(AP Photo/Alastair Grant)

Shirika la hali la hewa la Umoja wa Mataifa limechapisha rasimu ya uamuzi wa kisiasa uliotolewa na nchi katika mkutano wa COP26 uliofanyika huko Glasgow, Scotland.

Wapatanishi kutoka nchi karibu 200 watafanyia kazi rasimu hiyo iliyotolewa Jumatano ili kufikia makubaliano ya mwishio kabla mkutano kumalizika siku ya ijumaa.

Rasimu ya kwanza ya COP26 inahusu maamuzi yanayozitaka nchi kurejelea tena na kuimarisha malengo ya mwaka 2030 katika michango yao ya kitaifa kulingana na makubaliano ya Paris ya hali ya joto ifikapo mwaka 2022.

Matokeo yanaangaliwa kwa karibu kwa kile ambacho kinaweza kufanya nchi kuziba pengo kati ya malengo yao ya sasa ya hali ya hewa na hatua kubwa zaidi.

Hatua hizo wanasayansi wanasema zinahitajika kuzuia viwango vya maafa yanayotokea kufuatia ongezeko la joto.

XS
SM
MD
LG