Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:29

Idris Elba atoa wito kusaidiwa wakulima wadogo huko Glasgow

Mcheza filam Idris Elba alipokjuwa BFI Southbank, London August 21 2018. REUTERS/Henry Nicholls - RC1508128EE0
Mcheza filam Idris Elba alipokjuwa BFI Southbank, London August 21 2018. REUTERS/Henry Nicholls - RC1508128EE0

Mwigizaji wa Uingereza Idris Elba amepeleka nguvu yake ya msanii nyota kwenye mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa huko Glasgow Scotland kuangazia umuhimu wa kuwasaidia wakulima wadogo kukabiliana na ongezeko la joto duniani.

Elba na mkewe, mwanamitindo Sabrina Dhowre Elba, walipanda jukwaani leo Jumamosi kuunga mkono Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo wa Umoja wa Mataifa.

Elba alisema alitaka kuangazia hatari ya usambazaji wa chakula duniani kuingia matatani wakati wakulima wadogo hasa wanaokumbwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Alisema asilimia 80 ya chakula kinachotumiwa duniani kote kinazalishwa na wakulima wadogo.

"Mazungumzo haya kuhusu chakula ni jambo ambalo linalohitaji kupigiwa kelele na jambo moja ambalo nimejaaliwa ni mdomo mkubwa," Elba alisema.

Akizungumza kwenye jopo hilo hilo, mwanaharakati wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Uganda Vanessa Nakate, mwenye umri wa miaka 24, alisema ongezeko la joto duniani tayari linasababisha njaa kwa mamilioni ya watu duniani kote, ikiwa ni pamoja na katika nchi yake.

Alisema kuhama kutoka kwenye matumizi ya nyama na kwenda kwenye lishe inayotokana na mimea kunaweza kusaidia kuokoa mamilioni ya tani za uzalishaji wa gesi chafu kila mwaka huku kukitoa ardhi zaidi ambayo inatumika kwa chakula cha mifugo kwa sasa.

XS
SM
MD
LG