Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 17:29

Rais wa Misri kuhudhuria mkutano kuhusu Libya huko Ufaransa


Rais wa Misri Abdel Fatah Alsisi
Rais wa Misri Abdel Fatah Alsisi

Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi atahudhiria mkutano wa viongozi kuhusu Libya unaoandaliwa na rais Emmanual Macron wa Ufaransa hapo kesho Ijumaa na atafanya mazungumzo na rais wa Macron.

Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi atahudhiria mkutano wa viongozi kuhusu Libya unaoandaliwa na rais Emmanual Macron wa Ufaransa hapo kesho Ijumaa na atafanya mazungumzo na rais wa Macron.

Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa mataifa, Ujerumani na Italy, na unalengo la kuhakikisha uchaguzi ulopangwa kufanyika tarehe 24 Disemba mwaka huu nchini Libya unaendelea bila ya matatizo.

Misri ambayo inaangazia fursa za kiuchumi nchini Lyba na imerejesha harakati zake katika mji mkuu Tripoli, imetoa wito wa kufanyika uchaguzi licha ya malumbano kati ya makundi hasimu ya Libya kuhusu uchaguzi uliopangwa.

Misri iliunga mkono jeshi lenye makao yake mashariki mwa nchi chini ya uongozi wa Khalifa Haftar baada ya uchaguzi wa awali wa mwaka 2014 kuzusha mzozo na kuitawanya nchi kati ya makundi hasimu ya mashiriki na kaskazini mwa nchi.

XS
SM
MD
LG