Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 22:34

Shell yapata faida ya dola za Kimarekani bilioni 40, yakabiliwa na madai ya fidia


Wanaharakati na waandamanaji wakionyesha kero yao dhidi ya kampuni ya Shell London, Ijumaa, Aug. 28, 2020. (AP Photo/Alastair Grant)

Rekodi za mapato ya kampuni hiyo  ya Uingereza, Shell, imeongezeka zaidi ya mara mbili mwaka mmoja kabla, ikilingana na wale washindani wa Marekani mapema wiki hii...

Rekodi za mapato ya kampuni hiyo ya Uingereza imeongezeka zaidi ya mara mbili mwaka mmoja kabla, ikilingana na wale washindani wa Marekani mapema wiki hii na wana uhakika wa kuongeza msukumo kwa serikali mbalimbali kuendelea kuongeza kodi katika sekta hiyo.

“ Tunakusudia kuendelea kuwa na nidhamu wakati tunatoa mgao wa faida unaotulazimu kuwapa wenye hisa” Mtendaji Mkuu Wael Sawan alisema katika taarifa ya kiwango cha mapato ya kwanza tangu achukue madaraka Januari 1.

Shell pia imetoa rekodi ya faida katika kipindi cha robo ya nne cha dola bilioni 9.8, kufuatia unafuu mkubwa wa mapato yaliyotokana na mauzo ya gesi ya asili ya LNG, ikivuka utabiri uliofanywa na wachambuzi iliyokuwa faida ya dola bilioni 8.

Wakati huo huo zaidi ya wa Wanigeria 11,000 kutoka eneo linalozalisha mafuta la Niger Delta wamewasilisha madai ya fidia dhidi ya kampuni ya Shell katika Mahakama Kuu ya London, hatua mpya ya kesi hii ambayo itapima kama mashirika ya kimataifa yanaweza kuwajibishwa kwa vitendo vya kampuni zao tanzu zilizoko nje ya nchi.

Mnamo 2021, Mahakama ya Juu ya Uingereza iliruhusu kikundi cha watu 42,500 wakiwemo wakulima na wavuvi wa Nigeria kuishtaki Shell katika mahakama za Uingereza, baada ya miaka mingi ya uvujaji wa mafuta ambao umechafua ardhi na maji ya ardhini.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG