Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:57

Waziri Mkuu wa Uingereza Sunak apigwa faini kwa kutofunga mkanda wa gari


Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak

Msemaji wa Sunak amesema Waziri Mkuu huyo ameomba msamaha kwa "kosa lake" na anamsihi kila mtu kufunga mkanda wa kiti anapokuwa ndani ya gari

Waziri Mkuu wa Uingereza amepigwa faini kwa kutofunga mkanda wa kiti ndani ya gari huku akiangalia kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii akiwa nyuma ya gari kaskazini magharibi mwa Uingereza.

Wakati Rishi Sunak alipokuwa akiangalia video hiyo kwenye Instagram kosa lake la kutofunga mkanda ndani ya gari lilionekana bila kificho na watazamaji walilalamikia suala hilo kwa polisi wa Lancashire.

Polisi wa Lancashire walisema Ijumaa kwamba "Baada ya kuchunguza suala hili, leo tumempa faini kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 42 kutoka London."

Msemaji wa Sunak amesema Waziri Mkuu ameomba msamaha kwa "kosa lake" na anamsihi kila mtu kufunga mkanda wa kiti anapokuwa ndani ya gari.

Hii si mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu kukabiliana na sheria. Mwaka 2020 wakati alipokuwa waziri wa fedha Sunak pamoja na Waziri Mkuu wa wakati huo Boris Johnson walipigwa faini kwa kuvunja sheria zilizowekwa wakati wa kipindi cha COVID. Kushindwa kufunga mkanda wa kiti ndani ya gari nchini Uingereza unaweza kupata faini ya hadi dola 620.

XS
SM
MD
LG