Beterbiev mzaliwa wa Russia ameshinda kila pambano kati ya mapambano yake yote 18 kwa njia ya KO na ndiye bingwa pekee wa dunia mwenye uwiano wa ushindi wa asilimia 100 kwa njia hiyo ya KO.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 atapigana tena kupitia bendera ya Canada kama alivyofanya aliponyakua taji la WBO kutoka kwa Joe Smith Jr. kwenye ukumbi wa Madison Square Garden huko New York ambako alishinda kwa KO katika raundi ya pili Juni mwaka jana.
Mshindi huyo wa taji la WBC, WBO na IBF kutoka Dagestan aliwakilisha Russia wakati wa michuano ya olimpiki akiwa bondia wa ndondii za ridhaa aliyeng’aa katika michuano ya ridhaa na katika Michezo ya Olimpiki ya London mwaka 2012, lakini sasa anaishi Montreal na ana pasipoti ya Canada.