Iran imemnyonga raia wa Uingereza mwenye asili ya Iran, Ali Reza Akbari aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi wa zamani wa Iran ambaye alishitakiwa kwa kufanya ujasusi kwa ajili ya uingereza.
Shirika la habari la Iran, Mizan, limeeleza kuhusu kifo chake Jumamosi lakini haikuwa wazi haraka lini tukio la kunyongwa lilifanyika.
Alikamatwa mwaka 2019. Mapema wiki hii, shirika la habari la BBC Persia lilitoa taarifa ya sauti kutoka kwa Akbari akisema aliteswa na alilazimishwa kukubali makosa ya uhalifu ambayo hakuyafanya.
Uingereza na Marekani ilishauri iran kutokufanya maamuzi ya kumnyonga.
Hatua hiyo imezusha ukosoaji wa ndani na nje kwa Iran ikiwemo kutoka kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali.