Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 00:18

Ukraine: Shambulizi la Russia lalenga raia mjini Zaporizhzhia, 17 wapoteza maisha


Shambulizi la bomu katika makazi ya raia lililofanywa na Russia katika mji wa Zaporizhzhia.

Takriban watu 17 wameripotiwa kuuwawa katika shambulizi la bomu lililolenga raia usiku katika mji wa Zaporizhzhia uliopo kusini mashariki mwa Ukraine.

Darzeni zaidi ya watu waliripotiwa kujeruhiwa.

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya Jumamosi alilaani “kwa maneno makali” jaribio la Russia kukikamata kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia na walisema majeshi ya Russia lazima yaondoke kabisa kutoka katika kinu hicho na kurejesha udhibiti wa mtambo huo kwa Ukraine.

Mwakilishi wa juu wa mambo ya nje Josep Borrell amesema ukamataji wa kinu cha nishati ya nyuklia “ni kinyume cha sheria, na kisheria ni batili,” na alisema uwepo wa Shirika la Kimataifa la Atomiki (IAEA) katika mtambo huo na kutozuiliwa kuingia katika eneo hilo kunahitajika haraka kwa maslahi ya usalama wa Ulaya kwa jumla,”

Josep Borrell
Josep Borrell

Mapema Jumamosi, IAEA iliripoti kuwa kinu cha Zaporizhzhia, kikubwa kabisa Ulaya, kilikuwa kimepoteza chanzo cha nishati yake pekee ya nje kutokana na mashambulizi mapya yanayofanywa na Russia na imekilazimu kutegemea majenereta ya dharura ya dizeli.

Vinu vyote sita katika mtambo huo vimefungwa, lakini bado vinahitaji umeme kwa ajili ya kuvipooza na hatua nyingine za usalama wake. IAEA ilisema wahandisi wa mtambo huo wameanza kukarabati laini za umeme zilizoharibiwa.

Shirika la uangalizi wa nyuklia limesema kinu hicho kinachounganisha nguvu ya laini ya umeme ya kilovolt -750 ilizimwa kiasi cha saa saba usiku Jumamosi kwa saa za huko. Imenukuu taarifa rasmi kutoka Ukraine, na pia ripoti kutoka kwa wataalam wa IAEA walioko katika eneo hilo, ambalo linashikiliwa na majeshi ya Russia.

FILE PHOTO: Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Zaporizhzhia.
FILE PHOTO: Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Zaporizhzhia.

Mkuu wa IAEA Rafael Grossi anasafiri kuelekea Moscow kufanya mazungumzo katika siku zijazo kuhusu kuweka eneo la ulinzi kuzunguka kinu hicho cha nyuklia. Alikuwa nchini Ukraine Ijumaa na alikutana na Rais Volodymyr Zelenskyy kuhusu hali ilivyo. Kuhamisha umiliki wa kiwanda hicho kwa Russia, Grossi alisema, ni kukiuka sheria za kimataifa.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imemtangaza Jenerali Sergei Surovikin Jumamosi kuwa ni kamanda mpya kwa ujumla wa majeshi ya Kremlin yanayopigana nchini Ukraine. Lilikuwa tamko la kwanza rasmi kwa kamanda mmoja wa majeshi yote yanayopigana Ukraine tangu uvamizi wa Russia ulipoanza Februari 24.

Sergei Surovikin
Sergei Surovikin

“Kwa uamuzi wa waziri wa ulinzi wa serikali ya shirikisho ya Russia, Jenerali wa Jeshi Sergei Surovikin ameteuliwa kuwa kamanda wa muungano wa majeshi yote katika eneo la operesheni maalum ya kijeshi,” taarifa hiyo ilisema, ikitumia lugha ya Kremlin kwa uvamizi wa Ukraine.

Surovikin tangu mwaka 2017 aliongoza Majeshi ya Anga za Juu Russia. Mwezi Juni, aliteuliwa kusimamia majeshi ya Russia kusini mwa Ukraine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG