Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 06:28

Russia yatangaza rasmi kumiliki maeneo manne ya Ukraine


Rais wa Russia, Vladimir Putin.
Rais wa Russia, Vladimir Putin.

Rais wa Russia, Vladimir Putin Jumatano amesaini sheria ya kurasimisha umiliki wa maeneo manne ya Ukraine.

Hatua hiyo kwa kiwango kikubwa inashutumiwa kuwa ni kinyume cha sheria na ambayo imefanyika wakati vikosi vya Ukraine vikisonga mbele kwa mapambano ili kuchukuwa maeneo hayo yaliyo chini ya udhibiti wa Russia.

Hatua hizo za Russia zilipitishwa mapema wiki hii na bunge, kutambua maeneo ya Ukraine ya Donetsk, Luhansk, Zaporizhia, na Kherson kuwa ni himaya za Russia.

Russia iliweka maafisa baada ya kufanya kile ilichoita kura ya maoni katika maeneo hayo.

Ukraine na washirika wake wa magharibi pamoja na Umoja wa Mataifa zimepinga matokeo ya kura na hatua ya kutwaliwa kwa maeneo hayo kiujumla ikisema kura hizo zilifanyika chini ya mazingira ya vitisho na hayawakilishi maoni ya wengi.

XS
SM
MD
LG