Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:34

Moscow yasema gari iliyolipuka imesababisha moto Daraja la Crimea


Daraja la Crimea.
Daraja la Crimea.

Moto mkubwa uliosababishwa na bomu la kwenye  gari umelivunja  daraja kuu linalounganisha Crimea hadi Russia, eneo ambalo Russia ililichukua  mwaka 2014, Moscow iliripoti Jumamosi, bila ya mara moja kuliaumu Ukraine.

Daraja hilo la njia ya magari na treni, lilijengwa kwa amri za Rais wa Russia Vladimir Putin na kuzinduliwa mwaka 2018, lilikuwa ndio kiunganishi kikuu cha usafiri kwa ajili ya vifaa vya kijeshi kwa wanajeshi wa Russia wanaopigana nchini Ukraine, hususan upande wa kusini, na pia kuwasafirisha wanajeshi kuvuka upande wa pili.

Likipitia eneo la mlango wa bahari la Kerch , ni kivuko pekee kati ya eneo linalokaliwa kimabavu la Crimea na Russia.

“Leo majira ya saa 12:07 asubuhi upande wa barabara wa daraja la Crimea … gari lililokuwa na bomu lililipuka, na kusababisha matenka saba ya mafuta kushika moto wakati yalikuwa yakielekea Crimea kwa njia ya reli,” mashirika ya habari ya Russia yalinukuu kamati ya kupambana na ugaidi kitaifa ikielezea.

Msemaji wa Kremlin alisema Putin alikuwa ameamuru kuundwa tume kuchunguza mlipuko huo, mashirika ya habari ya Russia yaliripoti.

Mkuu wa bunge la kanda lililosimikwa na Russia huko Crimea, Vladimir Konstantinov, aliishutumu tukio hilo kuwa ni “uharibifu wa waukraine.”

Russia ilikuwa imesisitiza kuwa daraja hilo liko salama licha ya mapigano huko Ukraine lakini aliitishia Kyiv kulipiza visasi iwapo daraja hilo litashambuliwa.

Iwapo itathibitishwa kuwa Ukraine ilihusika na shambulizi, ni suala lenye wasi wasi mkubwa sana kwa Moscow kwa vile daraja hilo liko mbali na mstari wa mbele.

Kumekuwepo milipuko kadhaa katika votuo vya kijeshi vya Russia katika rasi ya Crimea.

Mafanikio ya karibuni ya Ukraine kukamata maeneo upande wa mashariki na kusini yamedumaza madai kutoka Kremlin wiki iliyopita kuwa walikuwa wamejiingiza Donetsk, jirani na Luhansk na mikoa ya kusini ya Zaporizhzhia na Kherson.

Maeneo hayo manne ni njia muhimu ya ardhini kati ya Russia na rasi ya Crimea, na kwa pamoja ni eneo la takriban asilimia 20 ya Ukraine.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG