Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:33

Zaidi ya watu 200,000 waandikishwa katika jeshi la Russia ndani ya wiki mbili


Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu
Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu

Zaidi ya watu 200, 000 wameandikishwa katika jeshi la Russia tangu Rais Vladimir Putin atangaze harakati za kuhamasisha watu kujiunga na jeshi hapo Septemba 21, waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu amesema Jumanne.

“Kufikia leo, zaidi ya watu 200, 000 wameingia jeshini, Shoigu amesema katika mkutano uliopeperushwa kwenye televisheni.

Uhamasishaji huo wa Russia kuomba watu kujiunga na jeshi unalenga kuimarisha vikosi vya Moscow nchini Ukraine.

Hatua hiyo ilitangazwa baada ya mfululizo wa matukio ya kushindwa kwa jeshi la Russia kwenye uwanja wa mapambano.

Kremlin ilisema uhamasishaji huo ni wa muda na unalenga kusajili wanaume 300,000.

Shoigu amesema wale wanaohamasishwa wanapewa mafunzo ya kijeshi kwenye vituo 80 kwenye uwanja na vituo sita vya mafunzo.

Uhamasishaji huo wa Kremlin ulisababisha baadhi ya maandamano na wanaume walio na umri wa kuingia jeshini kuondoka nchini, huku maelfu wakikimbilia katika nchi jirani, ambazo zilikuwa chini ya umoja wa kisoviet.

XS
SM
MD
LG