Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:43

Russia yafanya shambulizi katika makazi ya watu mjini Zaporizhzhia, Ukraine


Shambulizi lililofanywa na majeshi ya Russia katika jengo la makazi ya watu huko Zaporizhzhia, Ukraine, siku ya Alhamisi.
Shambulizi lililofanywa na majeshi ya Russia katika jengo la makazi ya watu huko Zaporizhzhia, Ukraine, siku ya Alhamisi.

Afisa wa Ukraine alisema Alhamisi Russia imeyashambulia kwa makombora  majengo ya makazi ya watu katika mji wa Zaporizhzhia, na kuua watu wawili.

Oleksandr Starukh, gavana wa mkoa wa Zaporizhzhia, alichapisha katika akaunti ya Telegram kuwa watu wengine watano walikuwa wamekwama katika kifusi kufuatia shambulizi hilo.

Jengo la makazi ya watu laharibiwa vibaya na kombora la Russia huko Zaporizhzhia.
Jengo la makazi ya watu laharibiwa vibaya na kombora la Russia huko Zaporizhzhia.

Ukraine inaendelea kuudhibiti mji huo, lakini sehemu kubwa ya mkoa wa Zaporizhzhia inakaliwa kimabavu na Russia.

Rais wa Russia Vladimir Putin amesaini sheria Jumatano inayotangaza kuwa Russia imejiingiza katika eneo la Zaporizhzhia na mikoa mingine mitatu, hatua iliyopingwa na Ukraine na washirika wake wa Magharibi, pamoja na Umoja wa Mataifa, wakieleza ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa.

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Zaporizhzhia ni makazi ya kinu kikubwa cha nishati ya nyuklia kwa Ulaya na mashambulizi katika miezi ya hivi karibuni imeongeza hofu ya kimataifa kuhusu maafa ya nyuklia kutokea.

Rafael Grossi, mkuu wa shirika la nguvu za atomiki la UN ataitembelea Kyiv na Moscow wiki hii kwa kile alichosema itakuwa ni mikutano muhimu. Amesema Jumatano kuwa kuna haja ya kulilinda eneo linalozunguka mtambo wa umeme “hivi sasa ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote ule.”

Zelenskyy asema Putin "ameemewa”

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya Jumatano usiku kuwa majeshi yake yamechukua tena Novovoskrysenske, Novohryhorivka, na Petropavlivka, vijiji vitatu katika mkoa wa Kherson ambao ulikuwa pia upo katika madai ya Russia kwamba wameyakamata.

Mafanikio hayo yanaongeza orodha ya mafanikio ya Ukraine ya hivi karibuni katika kuyarejesha maeneo katika himaya yake kutoka mikononi mwa Russia katika maeneo ya kaskazini mashariki na kusini mwa nchi hiyo.

Baadhi ya taarifa katika katika repoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG