Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 02:36

Majirani wa Russia wamefunga mipaka, maelfu ya raia wa Russia wanakimbia nchi yao


Raia wa Russia wanaokimbia nchi yao wakiwa kwa mpaka wa Russia na Georgia baada ya rais Putin kutaka raia wakijunge na jeshi na kwenda kupigana Ukriane. Sept 27 2022. Picha: AP
Raia wa Russia wanaokimbia nchi yao wakiwa kwa mpaka wa Russia na Georgia baada ya rais Putin kutaka raia wakijunge na jeshi na kwenda kupigana Ukriane. Sept 27 2022. Picha: AP

Serikali ya Finland imetangaza kwamba itafunga mpaka wake kesho ijumaa kwa watalii kutoka Russia, ikiwa ni nchi ya mwisho ya EU, Jirani wa Russia, kufanya hivyo.

Poland, Estonia, Latvia na Lithuania zilifunga mipaka yao mapema mwezi huu kwa watalii kutoka Russia.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Finland amesema kwamba watu kutoka Russia wanaruhusiwa kutembelea familia zao au kufanya kazi au kwa ajili ya masomo.

Hatua ya Finland imejiri baada ya idadi ya raia wa Russia wanaovuka mpaka na kuingia nchi Jirani kuongezeka kwa kazi sana baada ya rais wa Russia kuagiza raia kujiunga na jeshi ili kuendelea kupigana nchini Ukraine.

Putin ametangaza kutuma wanajeshi 300,000 wa akiba nchini Ukriane.

Foleni ndefu zinaenelea kuonekana mpakani, raia wa Russia wakikimbia nchi yao. Foleni pia zinaonekana kuingia Georgia ambayo haihitaji wasafiri kuwa na visa kuingia mipaka yake.

XS
SM
MD
LG