Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 05:27

Russia yasitisha usambazaji wa gesi kwa Bulgaria na Poland kulipiza kisasi


FILE PHOTO: Pipe ya gesi ya Siberia kutoka kiwanda cha nishati cha Gazprom katika stesheni ya kujaza gesi ya Atamanskaya nje ya mji wa mbali wa mashariki wa Svobodny.

Hatua hizo zimepingwa na viongozi wa Ulaya kama “ kuwarubuni” na zinakuja wakati nchi za Ulaya zimeungana na Marekani katika kuimarisha upelekaji wa shehena ya silaha ili kuisaidia Ukraine kukabiliana na shambulizi jipya la Russia katika eneo la mashariki.

Ukraine iliripoti Jumatano kwamba vikosi vya Russia vimefanikiwa katika baadhi ya vijiji huko.

Russia imeripoti idadi ya milipuko katika eneo lake kwenye mpaka, ikiwemo moshi kwenye hifadhi ya silaha ambayo Kyiv inaita Karma.

Moscow imesema kukata usambazaji wa gesi ni kuimarisha mahitaji yake ya malipo kwa sarafu ya rouble zinazohitajika kulinda uchumi wake dhidi ya vikwazo.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, alisema Russia ni msambazaji wa nishati wa kutegemewa na alikanusha kuwa ilikuwa inajihusisha na kurubuni.

Rais wa Russia Vladmir Putin mwezi uliopita alidai kwamba wanunuzi kutoka nchi zisizo rafiki walipie gesi kwa kutumia sarafu ya rouble au watakatiwa usambazaji.

Umoja wa Ulaya unasema hii inakiuka mikataba ambayo inataka malipo kwa njia ya Euro.

XS
SM
MD
LG