Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:31

Mfumuko wa bei wasababisha hali ngumu ya maisha Kenya


Kupanda kwa bei ya mafuta duniani. Bei yafikia dola 7.19 Marekani. (Photo by Patrick T. FALLON / AFP)
Kupanda kwa bei ya mafuta duniani. Bei yafikia dola 7.19 Marekani. (Photo by Patrick T. FALLON / AFP)

Kaya mbalimbali nchini Kenya zinakabiliwa na ukata wa kifedha baada ya bei za bidhaa muhimu kupanda kutokana na ongezeko la mfumuko wa bei, na kudhoofisha shilingi na kupandisha joto la Uchaguzi Mkuu Agosti 9.

Wachambuzi wa taasisi ya kifedha AZA Finance, wamesema ongezeko la mfumuko wa bei kutokana kupanda kwa bei za bidhaa katika soko la kimataifa limechangia sana katika sarafu ya eneo iliyodondoka kufikia kiwango kipya cha chini cha Ksh 114.55($1) dhidi ya dola wiki iliyopita kutoka Ksh114.33 wiki iliyopita.

Hali hiyo imechangiwa nah atua ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta kuongeza bei ya mafuta (petroli na diseli) kwa Ksh5 ($0.04) kwa lita.

“Wakati huo huo, joto la kisiasa linafukuta kabla ya uchaguzi wa mwezi Agosti. Kutokana na hali hii isiyotabirika na masuala ya mfumuko wa bei, tunatarajia thamani ya shilingi kuendelea kudhoofika katika kipindi kijacho,” wachambuzi hao wamesema kupitia ripoti yao ya kila siku juu ya hali ya soko iliyotolewa Machi 24.

Mafuta ghafi ulimwenguni ambayo yalifikia $130 kwa pipa Machi 8, yameshuka kufikia $121.02, kwa pipa Machi 24.

Wiki iliyopita, watengenezaji wa maziwa Kenya wameongeza bei kati ya Ksh2 ($0.01) na Ksh5 ($o.04) kwa paketi ya ml 500 ya aina ya maziwa freshi na chapa ya muda mrefu, ikiongeza orodha ya bidhaa za msingi ambazo zimeshuhudiwa bei zake kupanda katika wiki kadhaa za karibuni, ikwemo mkate, mafuta ya kula, sukari, unga wa ngano na mahindi. Bidhaa nyingine ambazo bei zake zimepanda ni chum ana simenti.

Jumuiya ya Wasafirishaji Kenya imewashauri wanachama wake nchi nzima kupitia tangazo lake la Machi 14 kuongeza bei ya usafirishaji kwa asilimia tano ili waweze kuendeleza biashara zao katika mazingira ya hivi sasa na kuepuka kuporomoka kabisa biashara zao.

Wiki iliyopita Umoja wa Walaji Kenya uliliomba bunge kufikiria kufuta kodi ya ongezeko la thamani katika gesi au kupunguza hadi asilimia 8 kutoka asilimia 16 hivi sasa.

Uvamizi wa Russia huko Ukraine umeyumbisha upatikanaji wa mafuta, mbolea na ngano ikipelekea ongezeko la gharama ya bidhaa hizo duniani kote.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African, Kenya.

XS
SM
MD
LG