Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 11:15

Uchumi wa dunia unatarajiwa kupungua kwa asilimia 2.6 kutokana na vita vya Ukraine.


James Zhan, mkurugenzi wa kitengo cha uwekezaji na biashara kwenye shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa mataifa (UNCTAD) akishiriki mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva. Februari 5, 2018. Picha ya Reuters.

Wachumi wa Umoja wa mataifa wanaonya kwamba matarajio ya ukuaji wa uchumi mwaka huu yanafifia kwa haraka kutokana na athari mbaya za vita nchini Ukraine.

Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa mataifa(UNCTAD) limeshusha sana makadirio ya awali yenye matumaini ya ukuaji wa uchumi wa dunia, kwa kuzingitia hali hiyo mpya.

Ripoti iliyosahihishwa ya UNCTAD kuhusu biashara na maendeleo inakadiria kuwa uchumi wa dunia utapungua kwa asilimia 2.6 mwaka huu wa 2022 kutoka madakirio ya asilimia 3.6 hapo awali. Shirika hilo linasema sababu kuu ya kushusha kwa kiasi kikubwa makadirio ya ukuaji wa uchumi, ni sintofamu inayozunguuka vita nchini Ukraine.

Ripoti hiyo inasema kiwango cha uharibifu wa kijeshi, muda wa vita na vikwazo dhidi ya Russia, kutaongeza kudorora kwa uchumi unaoendelea ulimwenguni na kudhoofisha afueni iliyoanza kupatikana baada ya janga la Covid 19.

Ripoti inasema Russia itakabiliwa na hali ya kudorora sana kwa uchumi mwaka huu.

Mkurungenzi wa kitengo cha UNCTAD kuhusu mikakati ya utandawazi na maendeleo Richard Kozul-Wright, anasema vita vya Ukraine huenda vikaongeza mivutano ya kisiasa kwenye ngazi ya kimataifa, kuamua sera za kitaifa za fedha, kuongeza madhara ya mfumuko wa bei na kusababisha ongezeko la bei ya mafuta na bidhaa nyingine. Anasema maeneo yote ya uchumi wa dunia yataathiriwa vibaya na mzozo wa Ukraine, wengine zaidi ya wengine.

“Umoja wa Ulaya utaona makadirio ya ukuaji wa uchumi wake yakishuka sana, lakini pia katika baadhi ya maeneo ya katikati na kusini mwa Asia. Na nchi ambazo zitaona makadirio kuhusu ukuaji wa uchumi wao hayashuki sana, mfano zile za kusini mwa Jangwa la Sahara, ziko katika hatari zaidi ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa kama tunavyoona katika nchi hizo ambazo ni waagizaji wakubwa wa chakula, hasa ngano”, amesema.

Kozul-Wright anasema kiwango kikubwa cha deni la nje kwa nchi maskini ni jambo linalotia wasiwasi.

Ripoti hiyo inakadiria kuwa nchi maskini zitahitaji dola bilioni 310 kulipa deni lao la nje mwaka huu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG