Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:15

Italy na Angola wametia saini mkataba wa usambazaji gesi


Mfano wa kiwanda cha gesi ambapo Italy na Angola wametia saini ili kuongeza usambazaji wa huduma ya gesi na kuacha kutegemea gesi kutoka Russia
Mfano wa kiwanda cha gesi ambapo Italy na Angola wametia saini ili kuongeza usambazaji wa huduma ya gesi na kuacha kutegemea gesi kutoka Russia

Italy siku ya Jumatano iliingia mkataba na Angola ili kuongeza usambazaji wa gesi kutoka nchi hiyo ya kusini mwa Afrika huku ikihangaika kujitenga haraka na gesi ya Russia kutokana na vita vya Ukraine.

Tamko la azma hiyo lilitiwa saini kuendeleza ubia mpya wa gesi asilia na kuongeza mauzo ya nje kwa Italy taarifa kutoka kwa waziri wa mambo ya nje wa Italy ilitangaza. Leo tumefikia makubaliano mengine muhimu na Angola ya kuongeza usambazaji wa gesi, Waziri wa Mambo ya Nje, Luigi Di Maio alisema katika taarifa hiyo.

Nia ya dhati ya Italy ya kutofautisha vyanzo vya usambazaji wa nishati imethibitishwa, Di Maio alisema mwishono mwa ziara ya saa mbili na nusu mjini Luanda.

Waziri Mkuu Mario Draghi anataka kuiongeza Angola na Congo-Brazzaville kwenye mpango wa wasambazaji kuchukua nafasi ya Russia ambayo inatoa takribani asilimia 45 ya gesi ya Italy. Hatutaki kutegemea tena gesi ya Russia kwa sababu utegemezi wa kiuchumi haupaswi kuwa utii wa kisiasa alisema Draghi katika mahojiano na gazeti la Corriere della Sera linalochapishwa kila siku ya Jumapili.

XS
SM
MD
LG