Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:50

Russia yapiga makombora katika makazi ya watu Ukraine, yaonya vita vitaongezeka


Watu waliowasili kutoka Kherson inayokaliwa na Russia kwa mabavu wakisubiri kusafirishwa kwenda Russia katika kituo cha treni cha Dzhankoi, Crimea, ambayo inakaliwa na Russia tangu mwaka 2014, Oct. 21, 2022, huku mwanajeshi wa Russia akisimamia zoezi hilo.
Watu waliowasili kutoka Kherson inayokaliwa na Russia kwa mabavu wakisubiri kusafirishwa kwenda Russia katika kituo cha treni cha Dzhankoi, Crimea, ambayo inakaliwa na Russia tangu mwaka 2014, Oct. 21, 2022, huku mwanajeshi wa Russia akisimamia zoezi hilo.

Ikiwa inakabiliwa na shinikizo upande wa kusini mwa Ukraine, Russia imefyatua makombora na kupeleka ndege zisizokuwa na rubani ndani ya eneo linaloshikiliwa na Ukraine la Mykolaiv siku ya Jumapili.

Shambulizi hilo limeharibu jengo la makazi ya watu katika mji unaotengeneza meli karibu na mstari wa mbele na kusema kuwa vita hivyo vinaelekea katika mgogoro “usioweza kudhibitiwa”.

Mykolaiv iko takriban km 35 kaskazini magharibi mwa mstari wa mbele kwenye eneo linalokaliwa kimabavu la Kherson, mkoa wa kusini ambapo Russia imeamuru watu 60,000 kukimbia shambulizi la Ukraine “ili muokoe maisha yenu.”

Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, ambaye baadhi ya wazalendo wa Russia wamemlaumu kwa Moscow kurejea nyuma katika vita tangu uvamizi wa Russia Februari 24, alizungumzia “hali inavyozidi kuwa mbaya” katika mawasiliano ya simu na mawaziri wenzake Ufaransa, Uingereza na Uturuki, wizara imesema.

Sergei Shoigu
Sergei Shoigu

Pia aliongea kwa simu na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin kwa mara ya pili katika siku tatu. Nyaraka ya mazungumzo ya simu za Petagon zilisema Austin alimwambia Shoigu yeye “alikataa sababu zozote zinazotolewa na Russia kuendeleza mgogoro huo.”

Bila ya kutoa ushahidi wowote, Shoigu alisema Ukraine ingeweza kuuzidisha mgogoro huo kwa kutumia “bomu chafu” -mabomu ya kawaida ambayo yamechanganywa na miale ya nyuklia. Ukraine haina silaha za nyuklia, wakati Russia alisema ina uwezo wa kuilinda himaya ya Russia kwa kutumia makombora ya nyuklia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alizipinga tuhuma hizo, akiziita “upuuzi” na “hatari”. Aliongeza kuwa: Russia mara kwa mara inawashutumu wengine kwa kile ambacho wamepanga kukifanya wao.”

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG