Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:36

Russia: Hali ni mbaya sana, Ukraine inapanga kutumia “bomu chafu”


Wanajeshi wa Russia wakiwa katika mazoezi ya usiku kusini mwa mji wa Rostov-on-Don
Wanajeshi wa Russia wakiwa katika mazoezi ya usiku kusini mwa mji wa Rostov-on-Don

Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, amemwambia mwenzake wa Ufaransa katika mazungumzo ya simu kwamba hali nchini Ukraine imeharibika sana na inaelekea kuwa hali “isiyoweza kudhibitiwa.”

Mazungumzo hayo ambayo yamechapishwa na serikali ya Russia, yanaeleza kwamba Shoigu amemwambia mwenzake wa Ufaransa kwamba wana wasiwasi mkubwa huenda Ukraine ikatumia “bomu chafu” katika vita hivyo.

Russia haijatoa ushahidi wowote kuonyesha kwamba Ukraine inaweza kutumia silaha kama hiyo.

"Wamezungumzia hali ilivyo nchini Ukraine ambayo inaendelea kuharibika kwa haraka,” imesema taarifa ya wizara ya ulinzi ya Russia na kuongezea kwamba “inaelekea kuwa mbaya kiasi cha kudhibitiwa.”

Wizara ya ulinzi haijatoa taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo.

XS
SM
MD
LG