Kyiv ilisema imewaua maafisa 34, akiwemo afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la majini Viktor Sokolov, katika shambulizi ambalo halijawahi kutokea wiki iliyopita kwenye makao makuu ya jeshi la majnii katika peninsula ya Crimea inayokaliwa na Russia.
Sokolov, akiwa amevalia sare, alionyeshwa kwa njia ya video akishiriki mkutano uliokuwa ukiongozwa na waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu.
Taarifa ya wizara ilisema mkutano huo ulifanyika siku hiyo asubuhi, lakini haikumtaja Sokolov.
Pia alionekana mara kadhaa kwenye picha ya video hiyo ya dakika nane iliyotolewa na wizara lakini Sokolov hakuonyeshwa akizungumza.
Kremlin iliwaambia waandishi wa habari muda mfupi kabla ya taarifa ya wizara hiyo kuwa "haina habari" kuhusu hali ya kamanda huyo na kuahirisha maswali kwa wizara ya ulinzi.
Jumanne jioni, vikosi maalum vya Ukraine vilisema "vilifafanua" maelezo kuhusu mashambulizi hayo ya wiki iliyopita.
“Wengi (maafisa waliouawa) bado hawajatambuliwa kwa sababu sehemu za miiili yao zimetawanyika,” walisema.
Shambulio hilo ni pigo kubwa kwa Moscow, ambayo imekumbwa na mashambulizi kadhaa kwenye bandari muhimu ya kimkakati ya Sevastopol katika miezi ya hivi karibuni.
Crimea ilichukuliwa na Russia mwaka 2014, na ni kitovu muhimu cha shughuli za jeshi la Moscow.
Chanzo cha habari ni shiriuka la habari la AFP
Forum