Wanajeshi wa Russia walivamia mji wa Beryslav, na kumuua mwanamke mmoja na kujeruhi wanawake watatu ikijumuisha afisa wa polisi, amesema.
Shambulizi lingine la anga lilimuua mwanaume mwenye umri wa miaka 67 katika kijiji cha Lvove, alisema Prokudin.
Mijni yote ipo katika upande wa Kherson wa Ukraine katika ukingo wa magharibi wa mto Dnipro.
Russia mara kwa mara hufanya mashambulizi katika miji na vijiji ikijumuisha mashariki mwa mji wa Kherson kutokea upande wa pili wa mto.
Ndani ya Russia, ndege isiyo na rubani ilishambulia jengo la utawala katika mji wa Kursk, na kuharibu kidogo paa gavana wa eneo Roman Starovoit aliripoti.
Forum