Vladimir Kara-Murza Jr, mwenye umri wa miaka 42, mapema wiki hii alihukumiwa kwa uhaini kwa kulaani hadharani vita vya Russia nchini Ukraine na kuhukumiwakifungo cha miaka 25 gerezani ikiwa ni sehemu ya mpango wa Kremlin kuwakandamiza wakosowaji wake.
Wakili wake Vadim Prokhorov amesema kupitia ujumbe wa Facebook, Jumapili, kwamba, mteja wake aliwasilishwa katika gereza la IK-6, lenye ulinzi mkali katika mji wa Omsk jimboni Siberia siku ya Alhamisi.
Kara-Murza ambaye ni mwanahabari na mwanaharakati wa upinzani, aliwekwa jela Aprili 2022.
Mashitaka dhidi yake yalitokana na hotuba aliyoitoa wiki kadhaa kabla katika baraza la wawakilishi la Arizona ambapo alitangaza kupinga uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Forum