Imedai kwamba uvamizi huo ulitekelezwa kwa kuzingatia madai ya uongo ya Russia kuhusu mauaji ya halaiki ya watu katika maeneo ya Luhansk na Donetsk, mashariki mwa Ukraine ili kutoa sababu ya Russia kuvamia Ukraine.
Ukraine inasisitiza kwamba mahakama ina uwezi, msimamo ambao unaongwa mkono na washirika wa Ukraine.
Maria Zabolotskaya, wakili wa Russia mahakamani, amesema kwamba madai ya Ukraine ni ya kisiasa na hayastahili kupewa thamani yoyote ya kisheria wakati wa kutafsiri mkataba kuhusu mauaji ya halaiki ya watu.
Huenda jopo maalum la mahakama likachukua wiki au miezi kadhaa kufikia uamuzi iwapo kesi hiyo inastahili kusikilizwa.
Chanzo cha habari hii ni AP
Forum