Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 20, 2025 Local time: 13:52

Rais Zelenskyy asema wawekezaji wa Marekani wapo tayari kuwekeza Ukraine


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, Jumapili amesema kwamba alikutana na wajasiriamali na wafadhili wa Kimarekani wakati wa ziara yake ya wiki nzima nchini Marekani.

Ameongeza kusema kwamba kutokana na mikutano hiyo majadiliano ya fursa za uwekezaji nchini Ukraine, yalijadiliwa.

Zelenskyy amesema wafanyabiashara ambao walijumuisha mabilionea Michael Bloomberg, Larry Fink, na Bill Ackman, walikua tayari kuwekeza katika miradi mikubwa ya kuikarabati Ukraine baada ya vita vyake dhidi ya Russia.

Kupitia mtandao wa Telegram, akiambatanisha na picha za mkutano wake, aliandika kwamba wafadhili na wajasiriamali wa Marekani wamemthibitishia kuwa wapo tayari kufanya uwekezaji mkubwa nchini humo mara baada ya kumalizika kwa vita na kupewa uhakika wa usalama.

Katika ziara yake ya Marekani, na Canada wiki iliyopita, rais Zelenskyy, ameendelea kusisitiza umuhimu wa msaada wa kijeshi na kifedha kwa Kyiv, katikka juhudi za kukabiliana na uvamizi wa miezi 19 wa Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG