Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 00:52

Ripoti ya CAR : Silaha bado zinaendelea kufika Sudan Kusini


Ripoti ya Conflict Armament Research - CAR

Pamoja na kuwepo mikakati ya udhibiti wa silaha kwa muda mrefu, silaha mpya zinaendelea kufika maeneo ya vita Sudan Kusini na mara kwa mara kupitia nchi jirani, kulingana na ripoti ya kina iliotolewa Alhamisi na kundi linalofuatilia silaha.

Uchunguzi wa miaka minne uliofanywa na Conflict Armament Research-CAR lenye makao yake London kuhusiana na upelekaji wa silaha ambazo zinasaidia kuendeleza vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan Kusini tangu Disemba 2013, imeeleza kuhusika kwa nchi jirani hususan Uganda katika kukwepa vikwazo vya silaha.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilikuwa halikuweka vikwazo vya silaha dhidi ya Sudan Kusini hadi Julai 2018, zaidi ya miaka minne ya kuwepo vita ambavyo viliuwa takribani watu 380,000.

Umoja wa Ulaya (EU) unapiga marufuku uuzaji silaha moja kwa moja unaofanywa na nchi wanachama kwenda Sudan tangu 1994, na imefanya mabadiliko kidogo ya marufuku ikijumuisha taifa jipya la Sudan Kusini lililojipatia uhuru mwaka 2011.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG