Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 12:41

Sudan Kusini yapinga kuundwa mahakama ya uhalifu wa vita


Wanajeshi wa Sudan Kusini wa jeshi la ukombozi la Sudan (SPLA)
Wanajeshi wa Sudan Kusini wa jeshi la ukombozi la Sudan (SPLA)

Afisa wa juu wa Sudan Kusini anasema serikali inapinga kuundwa kwa mahakama ya uhalifu wa vita, ambapo ni moja ya kipengele muhimu sana katika makubaliano ya amani yaliyofikiwa hivi karibun na pande zinazo zozana.

Mahakama hiyo inayo tarajiwa kuundwa itakuwa na mchanganyiko wa majaji wa Sudan Kusini na watalaamu wa uhalifu wa vita, ambao watakuwa na jukumu la kusimamia kesi za washukiwa wanao tuhumiwa kutenda ukatili wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya takriban miaka mitano nchini Sudan Kusini.

Wanaharakati wa jamii za kiraia wanasema ‘mahakama mchanganyiko’ ni vyema iundwe bila ya uchelewesho ili kumaliza hali ya watu kutohofia kushtakiwa nchini Sudan Kusini.

Lakini akiongea na wana habari mjini Juba hivi karibuni, waziri wa habari, Michael Makuei aliiitaja mahakama hiyo kuwa “nyenzo ya troika kubadili utawala’ wanachama wa troika ni Marekani, Uingereza na Norway.

Makuei amesema kitu chochote ambacho kinabainisha ni kikwazo kwa mkatabab wa amani hakikaribishwi, lakini amedai kwamba nchi za troika na taasisi nyingine za kikanda ni lazima ziweke kipaumbele kwa amani.

‘Mahakama hiyo ni nyenzo wanayotaka kuitumia dhidi ya watu wa Sudan Kusini, hasa uongozi wa Sudan Kusini. Wanataka kuitumia kwa dhana hiyo kwa vile mkatabab unatoa fursa ya kuundwa kwa mahakama hiyo ili kumshtaki mtu yoyote wakati wowote na mara ukishashtakiwa, unakamatwa na kupelekwa jela,” amesema Makuei.

Mwezi Septemba, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilidai kuwa utawala wa Kiir unapanga kuunda mahakama hiyo ili kuhakikisha kwamba watenda uhalifu, ikiwemo kusambaa kwa mauaji ya raia, wahusika wafikishwe mbele ya sheria. Human Rights Watch imekubaliana na wito huo.

Troika pia walizungumzia wasi wasi kuhusu msamaha wa karibuni uliotolewa na rais Kiir, ambao wanasema umevuruga utaratibu wa uwajibikaji.

Makuei amesema jumuiya ya kimataifa ni vyema ilenge katika kuleta amani endelevu kwa Sudan Kusini kwa kuhamasisha maridhiano, kuponya na kuishi pamoja kwa amani na kufikiria kuhsu uwajibikiaji hapo baadaye.

“badala ya kushinikiza kuundwa kwa mahakama hiyo, kwanini msiangalia utaratibu wa kulipa fidia na maelewano, na kuingia katika suala la maridhiano? Mara unapoanza mambo yote haya utakuwa unavunja mipango ya watu waliyonayo kwa ajili ya mahakama hii,” amesema Makuei.

Wanaharakati wa jamii za kiraia wamesema wa Sudan Kusini wanahitaji uwajibikiaji hivi sasa, uende sambamba na amani.

Jackline Nasiwa, mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Center for Inclusive Governance Peace and Justice lenye maka yake mjini Juba, ambaye alifanya kazi katika makubaliano ya amani, amesema hoja ya Makuei haina maana.

“Mjadala wa kusm amani kwanza na haki baadaye usije sasa, baada ya makubaliano ya amani kutiwa saini, kwasababu kimsingi kipengele cha tano ni sehemu ya makubaliano ya amani na ni vyema kitekelezwe kama kilivyo. Raia wanachotaka ni kumalizwa kwa hali ya watu kutokhofia kushtakiwa,” Nasiwa ameiambia VOA.

Kipengele cha tano katika mkataba wa amani uliyo fufuliwa kina zungumzia wazi kuhusu kuundwa kwa mahakama maalum pamoja na fidia na malipo kwa waathirika wa uhalifu uliotendwa wakati wa vita.

Nasiwa amesema utawala wa Kiir unajaribu kutoa dhana potofu kwamba mahakama maalum ni dhana ya nje.

James Okuk, mhadhiri wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Juba, amesema mahakama maalum ni sehemu muhimu sana ya mkataba ambao pande zote lazim uuheshimu.

“Baada ya miezi minane wakati serikali itakapoundwa, hapo ndipo tutafikiria kuwa na mahakama maalum kwa ajili ya Sudan Kusini na hautaliacha hilo kwasababu ni sehemu ya mkataba,” Okuk ameiambia VOA.

XS
SM
MD
LG