Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:31

Ramaphosa alikosoa Baraza la Usalama la UN


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (Johanna Geron, Pool Photo via AP)
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (Johanna Geron, Pool Photo via AP)

Afrika Kusini, taifa lenye ushawishi mkubwa Afrika limekuwa likishikilia msimamo wa kutoegemea upande wowote, na kuhimiza mazungumzo kama njia bora ya kumaliza mzozo huo licha ya hasira za Jumuia ya Kimatiafa.

Wakati Rais Ramaphosa akiwahutubia wanadiplomasia wa nchi yake kwa ajili ya mataifa ya kigeni mjini Pretoria amesema kwamba ugomvi huu wa Ukraine umebainisha mapungufu ya Baraza la Usalama katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda Amani na usalama wa kimataifa.

Kiongozi huyo amesema kwamba Baraza la Usalama linayawezesha mataifa makuu kutumia nguvu zao kuchukua maamuzi ambayo mara nyingine ni ya hatari kubwa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. (AP Photo/Bebeto Matthews)
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. (AP Photo/Bebeto Matthews)

Anasema mfumo wa hivi sasa wa baraza hilo umepitwa na wakati na hauwakilishi watu wote duniani, na haupendelei mataifa yenye uchumi unaonyanyukia.

Ametoa wito wa kuwepo na mfumo wa kuruhusu maamuzi kuchukuliwa kwa njia ya kidemokrasia ili baraza hilo liweze kutekeleza majukumu yake kwa haki na kuepukana na hali ya kukwama inayosababishwa na wajumbe wachache kabisa.

Rais Ramaphosa amekuwa akizungumza muda mfupi kabla ya baraza kuu la mmoja wa mataifa kupiga kura kuiondoa Russia kutoka baraza la haki za binadamu kufuatia tuhuma kwamba wanajeshi wa Russia wamewauwa raia katika mji wa Bucha huko Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor kwa upande wake amesema msimamo wa Afrika kusini wa kutopendelea upande wowote haumanishi kwamba wanaunga mkono uvamizi wa kijeshi wa Russia huko Ukraine ambao ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Bi Pandor Amelaani pia jinisi Jumuiya ya kimataifa ilivyojibu uvamizi huo kwa kuiwekea Russia vikwazo vikali ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika uhusiano wa kimataifa tangu baada ya vita vya pili vya dunia.

Ameongeza kusema kwamba hawajashuhudia hatua kama hizo za pamoja kuhusiana na migogoro mingine kama vile Yemen na ukanda wa Gaza. .

XS
SM
MD
LG