Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 07:42

Vikwazo zaidi: Familia ya Putin, Lavrov wabanwa, sawa na benki muhimu.


Rais wa Russia Vladmir Putin katika mojawapo ya vikao na maafisa wa serikali yake. PICHA: REUTERS

Marekani imewawekea vikwazo watu wa karibu na rais wa Russia Vladmir Putin wakiwemo biti wake wawili, waziri wa mambo ya nje, benki, Pamoja na kupiga marufuku raia wa Marekani kuekeza nchini Russia.

Hatua hiyo inatokana na uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.

Benki kuu ya Russia Sberbank ambayo inashikilia theluthi moja ya mali za Russia, na benki ya nne kwa ukubwa nchini Russia ya Alfabank pia zimeekewa vikwazo.

Binti wawili wa Putin, Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov na wanachama wa baraza la usalama la Russia nao wamewekewa vikwazo hivyo.

Biden atangaza vikwazo zaidi

Kupitia ujumbe wa Twiter, Biden amesema kwamba "nilieleza wazi kwamba Russia italipia kwa gharama ghali sana kutokana na uvamizi wake dhidi ya Ukraine hasa katika mji wa Bucha.”

Watu kadhaa walipatikana wameuawa katika mji wa Bucha baada ya wanajeshi wa Russia kutoka mji huo na kurudi chini ya udhibithi wa jeshi la Ukraine.

“Hii leo, Pamoja na washirika wetu, tuatangaza awamu mpya ya vikwazo vibaya sana,” amesema Biden.

Russia, ambayo imesema kwamba ilianzisha “oparesheni spesheli” nchini Ukraine Feb 24, imekanusha madai ya kuwalenga raia na kuongezea kwamba picha zilizotolewa ni za “kughushi” na wala mauaji hayakutokea. Imesema kwamba picha hizo zimetengenezwa na mataifa ya magharibi.

Benki ya Sberbank, inamilikiwa na serikali na ndio mfadhili mkubwa wa serikali ya Russia. Benki ya Alfabank hata hivyo imesema kwamba vikwazo hivyo havitaathiri shughuli zake.

Raia wa Marekani wapigwa marufuku kuekeza Russia

White house imesema kwamba rais Biden amesaini amri ya kiutendaji “kupiga marufuku raia wa Marekani kuekeza nchini Russia, hatua ambayo itaitenga zaidi Russia na uchumi wa dunia.”

“ukweli ni kwamba nchi hiyo inaingia katika mgogoro mkubwa wa uchumi na kifedha Pamoja na wa kiteknolojia kwa kutengwa, na kwa namna hii, itarudi katika hali ya maisha ilicyokuwa wakati wa muungano wa kisovieti ilivokuwa miaka ya 1980.” amesema afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Biden.

Vikwazo zaidi kutangazwa Alhamisi, nanaokiuka washitakiwa

Wizara ya sheria ya Marekani imewafungulia mashtaka raia wa Russia oligarch Konstantin Malofeyev kwa kukiuka vikwazo vilivyowekewa Russia kutokana na uvamizi wake dhidi ya Ukraine.

Mwanasheria mkuu Merrick Garland, amesema kwamba wameharibu mtandao wa udukuzi unaosimamiwa na jeshi la ujasusi la Russia unaojulikana kama “botnet”.

Marekani vile vile inalenga kuwekea vikwazo zaidi katika hatua imetajwa kama ya “kulemeza taasisi zinazomilikuwa na serikali ya Russia” na kwamba hatua hiyo itahakikisha kwamba Kremlin haina uwezo wa kufadhili juhudi zake za vita

White house imesema kwamba taasisi hizo zitatajwa alhamisi wiki hii.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG