Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:29

UN yatahadharisha Libya kukabiliwa na ukosefu wa uthabiti


Mkuu wa masuala ya  kisiasa katika UN Rosemary DiCarlo (Picha na UN)
Mkuu wa masuala ya  kisiasa katika UN Rosemary DiCarlo (Picha na UN)

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa hali ya sasa ya mivutano inayoshuhudiwa nchini Libya inaweza kusababisha ukosefu wa uthabiti na kuundwa serikali mbili nchini humo.

Mkuu wa masuala ya kisiasa katika UN Rosemary DiCarlo ameliambia Baraza la Usalama la umoja huo kwamba juhudi zinachukuliwa kuisaidia Libya.

DICarlo amesema: "Uongozi wa Liby aunakabiliwa na mgogoro ambao kama hautasuluhishwa, unaweza kusababisha ukosefu mkubwa wa uthabti na kuepelekea kuundwa kwa serikali mbili nchini humo. Umoja wa mataifa unafanya juhudi kubwa kusuluhisha mgogoro huo. Tunalenga kuwaleta pamoja wadau wa Libyta wakubaliane katika misingi ya kikatiba, kuandaa uchaguzi mkuu haraka iwezekanavyo."

DiCarlo amesema kwamba hali ya Libya kwa sasa ni ya utulivu lakini kuna hali ya wasiwasi kutokana na matamshi makali na mivutano ya kisiasa.

Mgogoro wa sasa wa Libya ulianza baada ya kuahirishwa kwa cuhaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika Desemba tarehe 24 baada ya kushindwa kufikia makubaliano kuhusu sheria za uchaguzi na wagombea wa urais.

Karibu wapiga kura milioni 3 wamesajiliwa kushiriki zoezi hilo.

Mapigano na kuingiliwa na nchi za nje yametajwa kuwa sababu kuu zinazochangia kukosekana kwa hali ya utulivu nchini Libya, tangu kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi, mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG