Chirac alifariki mapema Alhamisi asubuhi akiwa na familia yake , mwanawe wa kambo ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP.
Marehemu Chirac alitumikia miaka miwili katika wadhifa wa urais wa Ufaransa na kuliongoza taifa lake kuingia katika sarafu moja ya Ulaya.
Bunge la Ufaransa lilisimamisha shughuli zake kwa dakika moja kwa kunyamaza kimya ikiwa ni kumuenzi na kutoa heshima zao kwa kiongozi huyo.