Idadi ya waandamanaji imepungua sana na hasa ghasia na mapambano yaliozuka wiki ilyiopita wakati polisi mjini Paris wakijitahidi kuleta utulivu. Wachambuzi wanasema huenda kupungua kwa ghasia ni kwa sababu za sikukuu ya Kritsmasi.
Akizungumza wakati anawatembelea wanajeshi wa Ufaransa wanaotumika katika kikosi cha kupambana na ugaidi huko Chad, Rais Macron alisema ni lazima hivi sasa pawe na utulivu, kuheshimu utawala na maelewano kwani nchi anasma inahitaji hali hiyo.
Katika hotuba yake hii leo Rais Macron alikosowa pia maamuzi ya Rais Trump kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Syria akisema mshirika wa karibu hana budi kuaminika.
Kiongozi huyo wa Ufaransa alitoa heshima zake pia kwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani aliyejiuzulu Jenerali Jim Mattis, akisema kwa muda wa mwaka walofanya kazi ameweza kushuhudia jinsi alivyokuwa mtu wa kutegemewa.
Baada ya mkutano na waandishai habari Rais Macron alikutana na viongozi wa wanawake katika ukumbi wa jingo la wanawake mjini N’Djamena na kutoa wito kwa wanawake na wasichana kuwezeshwa.
Macron anasema wanawake katika bara la Afrika wako nyuma katika mambo mengi na hivyo kunahitajika mkakati wa kuwawezesha ili hatimae wawe uhuru, mafanikio na maarifa barani Afrika.
Macron amesema “ sijaja hapa kutowa hotuba kubwa. Nimekuja kukuambieni kwamba nina amini nyinyi ni kitu kimoja
Mojawapo ya ufungo wa malengo yetu ya pamoja, ni kufanikiwa katika kuwawezesha wasichana na wanawake vijana”.